Mdo 24:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akatelemka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza liwali habari za Paulo.

2. Naye alipoitwa, Tertulo akaanza kumshitaki, akisema,Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa maangalizi yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili,

3. basi tunayapokea kila wakati na kila mahali, kwa shukrani yote.

4. Lakini nisikuudhi zaidi, nakusihi utusikilize maneno machache kwa fadhili zako.

Mdo 24