Mdo 23:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi.

2. Kuhani Mkuu Anania akawaamuru wale waliosimama karibu naye wampige kinywa chake.

3. Ndipo Paulo akamwambia, Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Wewe umeketi kunihukumu sawasawa na sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria?

4. Wale waliosimama karibu wakasema, Je! Unamtukana Kuhani Mkuu wa Mungu?

Mdo 23