Mdo 2:6-15 Swahili Union Version (SUV)

6. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

7. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?

8. Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?

9. Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia,

10. Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,

11. Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.

12. Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?

13. Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

14. Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15. Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;

Mdo 2