Mdo 16:29-36 Swahili Union Version (SUV)

29. Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;

30. kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

31. Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

32. Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.

33. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.

34. Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.

35. Kulipopambauka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.

36. Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Makadhi wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani.

Mdo 16