Mdo 16:2-8 Swahili Union Version (SUV)

2. Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio.

3. Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani.

4. Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike.

5. Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.

6. Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.

7. Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,

8. wakapita Misia wakatelemkia Troa.

Mdo 16