Mdo 11:3-12 Swahili Union Version (SUV)

3. wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.

4. Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema,

5. Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.

6. Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.

7. Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.

8. Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu.

9. Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.

10. Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni.

11. Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.

12. Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;

Mdo 11