Lk. 7:14-21 Swahili Union Version (SUV)

14. Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.

15. Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.

16. Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake.

17. Habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote, na katika nchi zote za kando kando.

18. Wanafunzi wa Yohana wakamletea habari za hayo yote.

19. Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

20. Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

21. Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.

Lk. 7