Lk. 4:6-11 Swahili Union Version (SUV)

6. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.

7. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

8. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

9. Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini;

10. kwa maana imeandikwa,Atakuagizia malaika zake wakulinde;

11. na ya kwamba,Mikononi mwao watakuchukua,Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

Lk. 4