Lk. 4:11-24 Swahili Union Version (SUV)

11. na ya kwamba,Mikononi mwao watakuchukua,Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

12. Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

13. Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.

14. Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.

15. Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.

16. Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.

17. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,

18. Roho wa Bwana yu juu yangu,Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,Na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa,

19. Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

20. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.

21. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.

22. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?

23. Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.

24. Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe.

Lk. 4