Lk. 4:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,

2. akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.

3. Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.

4. Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.

5. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.

Lk. 4