48. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.
49. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
50. Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki.
51. Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.
52. Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu.
53. Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.