Lk. 22:7-17 Swahili Union Version (SUV)

7. Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka.

8. Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila.

9. Wakamwambia, Wataka tuandae wapi?

10. Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye.

11. Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu?

12. Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo.

13. Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka.

14. Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye.

15. Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu;

16. kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.

17. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi;

Lk. 22