Lk. 22:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka.

2. Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu.

3. Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.

4. Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.

5. Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha.

6. Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.

7. Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka.

8. Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila.

Lk. 22