Lk. 21:27-35 Swahili Union Version (SUV)

27. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

28. Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.

29. Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.

30. Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.

31. Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.

32. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.

33. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

34. Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;

35. kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.

Lk. 21