1. Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.
2. Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.
3. Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;
4. maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.
5. Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema,
6. Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.