Lk. 20:37-47 Swahili Union Version (SUV)

37. Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.

38. Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.

39. Waandishi wengine wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema;

40. wala hawakuthubutu kumwuliza neno baada ya hayo.

41. Akawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi?

42. Maana, Daudi mwenyewe asema katika chuo cha Zaburi,Bwana alimwambia Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,

43. Hata niwaweke adui zakoKuwa kiti cha kuwekea miguu yako.

44. Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake?

45. Na watu wote walipokuwa wakimsikiliza, aliwaambia wanafunzi wake,

46. Jilindeni na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni.

47. Wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu.

Lk. 20