2. Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.
3. Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.
4. Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;
5. ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.