Lk. 2:12-21 Swahili Union Version (SUV)

12. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.

13. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,

14. Atukuzwe Mungu juu mbinguni,Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.

15. Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.

16. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.

17. Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.

18. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.

19. Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.

20. Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.

21. Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.

Lk. 2