39. Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.
40. Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza,
41. Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.
42. Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya.
43. Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.