Lk. 18:37-41 Swahili Union Version (SUV)

37. Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.

38. Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.

39. Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.

40. Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza,

41. Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.

Lk. 18