Lk. 18:35-43 Swahili Union Version (SUV)

35. Ikawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka;

36. na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini?

37. Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.

38. Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.

39. Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.

40. Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza,

41. Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.

42. Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya.

43. Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.

Lk. 18