32. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate;
33. nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.
34. Walakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.
35. Ikawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka;
36. na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini?
37. Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.
38. Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.
39. Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.
40. Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza,