23. Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi.
24. Yesu alipoona vile alisema, Kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu!
25. Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
26. Nao waliosikia walisema, Ni nani basi awezaye kuokoka?
27. Akasema, Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu.
28. Petro akasema, Tazama, sisi tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata.
29. Akawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu,
30. asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.