Lk. 17:32-36 Swahili Union Version (SUV)

32. Mkumbukeni mkewe Lutu.

33. Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.

34. Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

35. Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. [

36. Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]

Lk. 17