Lk. 16:27-31 Swahili Union Version (SUV)

27. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28. kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

31. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Lk. 16