Lk. 15:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize.

2. Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.

3. Akawaambia mfano huu, akisema,

4. Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?

5. Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.

6. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.

Lk. 15