Lk. 14:27-34 Swahili Union Version (SUV)

27. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

28. Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

29. Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

30. wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.

31. Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?

32. Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.

33. Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

34. Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?

Lk. 14