Lk. 14:1-13 Swahili Union Version (SUV)

1. Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.

2. Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura.

3. Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo?

4. Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake.

5. Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?

6. Nao hawakuweza kujibu maneno haya.

7. Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,

8. Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,

9. akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.

10. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.

11. Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

12. Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.

13. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,

Lk. 14