76. Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu,Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake;
77. Uwajulishe watu wake wokovu,Katika kusamehewa dhambi zao.
78. Kwa njia ya rehema za Mungu wetu,Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,
79. Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti,Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.
80. Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.