67. Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema,
68. Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.
69. Ametusimamishia pembe ya wokovuKatika mlango wa Daudi, mtumishi wake.
70. Kama alivyosema tangu mwanzoKwa kinywa cha manabii wake watakatifu;
71. Tuokolewe na adui zetuNa mikononi mwao wote wanaotuchukia;
72. Ili kuwatendea rehema baba zetu,Na kulikumbuka agano lake takatifu;
73. Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,
74. Ya kwamba atatujalia sisi,Tuokoke mikononi mwa adui zetu,Na kumwabudu pasipo hofu,
75. Kwa utakatifu na kwa hakiMbele zake siku zetu zote.
76. Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu,Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake;