52. Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;Na wanyonge amewakweza.
53. Wenye njaa amewashibisha mema,Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
54. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;Ili kukumbuka rehema zake;
55. Kama alivyowaambia baba zetu,Ibrahimu na uzao wake hata milele.
56. Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.
57. Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia, alizaa mtoto mwanamume.
58. Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye.
59. Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria.
60. Mamaye akajibu akasema La, sivyo; bali, ataitwa Yohana.
61. Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo.