Lk. 1:46-56 Swahili Union Version (SUV)

46. Mariamu akasema,Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

47. Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

48. Kwa kuwa ameutazamaUnyonge wa mjakazi wake.Kwa maana, tazama, tokea sasaVizazi vyote wataniita mbarikiwa;

49. Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,Na jina lake ni takatifu.

50. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizaziKwa hao wanaomcha.

51. Amefanya nguvu kwa mkono wake;Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52. Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;Na wanyonge amewakweza.

53. Wenye njaa amewashibisha mema,Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

54. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;Ili kukumbuka rehema zake;

55. Kama alivyowaambia baba zetu,Ibrahimu na uzao wake hata milele.

56. Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.

Lk. 1