Law. 6:18-23 Swahili Union Version (SUV)

18. Kila mwana mume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu awaye yote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu

19. BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

20. Matoleo ya Haruni na wanawe watakayomtolea BWANA, katika siku atakayotiwa mafuta, ni haya; sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga daima, nusu yake asubuhi, na nusu yake jioni.

21. Utaandaliwa kaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA.

22. Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa BWANA kwa amri ya milele.

23. Tena kila sadaka ya unga ya kuhani itateketezwa kabisa; isiliwe.

Law. 6