3. Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa BWANA itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,
4. na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.
5. Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.
6. Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu.
7. Kama akimtoa mwana-kondoo kuwa matoleo yake, ndipo atakapomtolea BWANA;