1. Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng’ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya BWANA.
2. Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.
3. Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa BWANA itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,
4. na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.