1. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2. Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtu atakapoondoa nadhiri, hizo nafsi za watu zitakuwa kwa BWANA, kama utakavyowahesabia wewe.
3. Na hesabu yako itakuwa kwa mtu mume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu.
4. Kama ni mwanamke, hesabu yako itakuwa shekeli thelathini.