Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote.