14. Na siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, naye atakwenda mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania, naye atampa kuhani hao ndege;
15. na kuhani atawasongeza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho mbele za BWANA kwa ajili ya kisonono chake.
16. Na mtu ye yote akitokwa na shahawa yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
17. Na kila nguo, na kila ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni.