Kut. 6:19-30 Swahili Union Version (SUV)

19. Na wana wa Merari; ni Mali, na Mushi. Hizi ni jamaa za hao Walawi sawasawa na vizazi vyao.

20. Huyo Amramu akamwoa Yokebedi ndugu ya baba yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia na thelathini na saba.

21. Na wana wa Ishari; ni Kora, na Nefegi, na Zikri.

22. Na wana wa Uzieli; ni Mishaeli, na Elisafani, na Sithri.

23. Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, umbu lake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

24. Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora.

25. Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za mababa ya Walawi sawasawa na jamaa zao.

26. Hawa ni Haruni ye yule, na Musa ye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao.

27. Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa ye yule, na Haruni ye yule.

28. Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri,

29. BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo.

30. Musa akanena mbele ya BWANA, Mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara, Farao atanisikizaje?

Kut. 6