Kut. 39:34-38 Swahili Union Version (SUV)

34. na kifuniko chake cha ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na kifuniko cha ngozi za pomboo, na pazia la sitara;

35. na sanduku la ushuhuda, na miti yake, na kiti cha rehema;

36. na meza, na vyombo vyake vyote, na mikate ya wonyesho;

37. na kinara cha taa safi, na taa zake, hizo taa za kuwekwa mahali pake, na vyombo vyake vyote, na mafuta ya taa,

38. na madhabahu ya dhahabu, na mafuta ya kutiwa, na uvumba mzuri, na pazia kwa mlango wa hema;

Kut. 39