11. yaani, hiyo maskani na hema yake, na kifuniko chake, na vifungo vyake, na mbao zake, na mataruma yake, na viguzo vyake, na matako yake;
12. hilo sanduku, na miti yake, na hicho kiti cha rehema, na lile pazia la sitara;
13. na hiyo meza, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na hiyo mikate ya wonyesho;
14. na hicho kinara cha taa kwa mwanga, na vyombo vyake, na taa zake, na hayo mafuta kwa nuru;