Naye akachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; na Musa akainuka na mapema asubuhi, naye akakwea katika mlima wa Sinai, kama BWANA alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake.