43. Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo, na hiyo Hema itafanywa takatifu na utukufu wangu.
44. Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu; pia Haruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
45. Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao.
46. Nao watanijua kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao; ni mimi BWANA Mungu wao.