Kut. 23:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu.

2. Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;

3. wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake.

4. Ukimwona ng’ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena.

Kut. 23