Kut. 22:17-26 Swahili Union Version (SUV)

17. Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.

18. Usimwache mwanamke mchawi kuishi.

19. Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.

20. Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye BWANA peke yake, na angamizwe kabisa.

21. Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

22. Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.

23. Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,

24. na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.

25. Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.

26. Ikiwa wewe kwa njia yo yote wapokea nguo ya jirani yako rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa;

Kut. 22