Ng’ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng’ombe ataachiliwa.