1. Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2. Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6. nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;