Kut. 1:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo.

2. Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda;

3. na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini;

4. na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri.

5. Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.

6. Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile.

7. Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.

Kut. 1