15. kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.
16. Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa.
17. Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza.
18. Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako,
19. ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema BWANA.
20. Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N’nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu?
21. Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;