19. Watayaita mataifa waje mlimani;Wakasongeze huko sadaka za haki;Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari,Na akiba zilizofichamana za mchangani.
20. Na Gadi akamnena,Na abarikiwe amwongezaye Gadi;Yeye hukaa kama simba mke,Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
21. Akajichagulia sehemu ya kwanza,Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;Akaja pamoja na wakuu wa watu,Akaitekeleza haki ya BWANA,Na hukumu zake kwa Israeli.
22. Na Dani akamnena,Dani ni mwana-simba,Arukaye kutoka Bashani.
23. Na Naftali akamnena,Ee Naftali, uliyeshiba fadhili,Uliyejawa na baraka ya BWANA;Umiliki magharibi na kusini.